Ripoti ya shirika la habari la Ahull Bayt(as)-ABNA- Taifa la Iran ni ngangari litajitosa katika kila nyanja kwa umoja na mshikamano tarehe 10 February kubatilisha tena njama za adui za kutaka kutenganisha baina ya wananchi, Mapinduzi ya Kiislamu na utawala wa Kiislamu hapa nchini.
Mkutano huo ulifanyika sambamba na kumbukumbu ya siku ya kihistoria ambapo kundi moja la wanajeshi wa kikosi cha anga lilojitenga na utawala wa Shah kumuunga mkono Imam Khomeini.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu alizungumzia matamshi kauli za viongozi wa Marekani eti wapo tayari kufanya mazungumzo na Iran, Alisema, matamshi na kauli hazo si jambo jipya na yamekuwa yakikaririwa kila siku, taifa la Iran limekuwa likitoa jibu kwa matamshi hayo kwa mujibu wa hatua za kivitendo za Wamarekani. Aidha maneno ya viongozi wa Marekani wanaodai kua sasa mpira uko katika uwanja wa Iran na kusema, sivyo hivyo bali mpira uko katika uwanja wa Marekani, kwani wanapaswa kujibu swali kwamba, pendekezo la kutaka kufanya mazungumzo na Iran sambamba na kudumisha vitisho lina maana gani?
Alisema: Mazungumzo hufanyika kwa minajili ya kuonesha nia njema na Marekani inafanya mambo kwa nia mbaya na baadae yaadai kwa maneno tu kua inataka kufanya mazungumzo! Amehoji kwamba je, taifa la Iran kutokana na yote hayo linaweza kuwa na imani kwamba mna nia nzuri?
Alibainisha sababu za kutolewa pendekezo na Marekani la kutaka kufanya mazungumzo na Iran, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema: “Tunaelewa haja yao ya kutaka kufanya mazungumzo kwa sababu siasa za Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati zimefeli na sasa Wamarekani wanatafuta karata ya turufu kwa ajili ya kufidia kushindwa huko.”
Alisema: kuivuta Jamhuri ya Kiislamu na mapinduzi ya wananchi wa Iran katika meza ya mazungumzo ndio karata ya turufu inayohitajiwa na Wamarekani, na wanataka kujidhihirisha mbele ya dunia kua wana nia njema na kwamba hakuna mtu anayeona nia yao.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliashiria kua pendekezo hilo lililotolewa miaka 4 iliyopita na Marekani kutaka kufanya mazungumzo na Iran, wakati huo huo ilisisitizwa na kuelezwa kua Tehran haitatoa maamuzi ya haraka na itasubiri kuona vitendo vya viongozi wa Washington, ila katika kipindi cha miaka 4 iliyopita hakujashuhudiwa isipokuwa kuendelezwa njama za aina mbalimbali, misaada ya Washington kwa magenge yanayofanya fitina na uungaji mkono kwa magaidi wanaotekeleza mauaji dhidi ya wasomi wa taifa la Iran.
Ayatullah Khamenei: “Mlisema kua mnatuwekea vikwazo vitakavyolilemaza taifa la Iran, je hicho ni kielelezo cha nia njema au nia mbaya?”
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu alisisitiza kwa kusema: “Mimi si mwanadiplomasia bali ni mwanamapinduzi, na kwa sababu hiyo ninasema waziwazi, kwa ukweli na kwa msimamo imara kwamba, mazungumzo yatakuwa na maana pale upande wa pili utakapoonesha nia njema.”
Akiwambia viongozi wa Warekani: Mnashika silaha mikononi mbele ya taifa la Iran kisha mwasema ima mazungumzo au risasi! Mwapaswa kuelewa kua taifa la Iran kamwe halitatishwa na mambo kama hayo.
Aidha alikosowa fikira ya baadhi ya watu wanaofurahia pendekezo la Marekani kutokana na ujahili wao au kutokuwa na malengo maalumu, alisema: kufanya mazungumzo na Marekani hakuwezi kutatua lolote kwani katika kipindi chote cha miaka 60 iliyopita Marekani hakutekeleza hata ahadi yake moja, mfano wa Mapinduzi yaliyopangwa na Marekani dhidi ya serikali ya Dr. Musaddiq nchini Iran ukizingatia ya kwamba Musaddiq alikuwa amewaamini Wamarekani, na uungaji mkono wa Washington kwa serikali ya kidhalimu na kidikteta ya Shah Pahlavi. Na baada ya Mapinduzi ya Kiislamu pia kuna wakati viongozi wa nchi waliwaamini Wamarekani na badala yake Washington iliitaja Iran kuwa ni mhimili wa shari na kulivunjia heshima taifa la Iran.
Aidha alisema kua: Mtu yeyote anayetaka kurejesha udhibiti wa Marekani hapa nchini na akapuuza maslahi ya kitaifa, maendeleo ya nchi na kujitawala kwa taifa kwa ajili ya kuridhisha Marekani atakabiliwa na mkono wa wananchi na kupingwa na wananchi iwapo atachukua msimamo kinyume na matakwa yao.
Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa taifa la Iran ni watu wapole na wanaopenda amani na kuongeza kuwa, Tehran inafanya mazungumzo na nchi zote ambazo hazifanyi njama dhidi ya Iran na suala hilo linahudumia maslahi ya taifa.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Harakati kubwa ya wananchi wa Iran ina lengo la kudhamini maslahi ya Iran, Umma wa Kiislamu na jamii ya mwanadamu kwa ujumla.
Alimazia kwa kusema: Katika siku za usoni nitazungumza viongozi kunako kadhia hiyo na kuwahimiza viongozi wote kuweka kando hitilafu zao na kuwa na kauli moja.
Mwanzo wa mkutano huo Meja Jenerali rubani Shah Saffi ambaye ni Kamanda wa Jeshi la Anga la Iran aliadhimisha siku ya Jeshi la Anga tarehe 7/feb/2013 ambayo inakumbusha tukio la kihistoria la makamanda wa jeshi hilo kumuunga mkono Imam Khomeini na akatoa ripoti kuhusu uwezo wa ndani na maendeleo yaliyopatikana katika Jeshi la Anga.